Thursday, July 18, 2013

KUOTEA KATIKA MPIRA WA MIGUU

        Elimu ya mpira wa miguu ni elimu ambayo muhusika humwingia taratibu.
Siku hadi siku.Upo mtata mkubwa sana wakati wa mchezo huu hasa pale linapopatikana goli na kumbe goli hilo ni la kuotea.

IKO HIVI
(1)Kitendo cha mchezaji kuwa karibu na goli la mpinzani wake kuliko mpira na beki wa pili wa mwisho.(Second last defender)
-Mchezaji huyo atakuwa ameotea.
(2)Kupata faida kwa kuwa eneo hilo.
-Mchezaji huyu alikuwa kaotea muda mrefu kabla hata ya mpira kupigwa, na kumfikia,huyo atakuwa ameotea.Kwani atapata faida ya kufunga goli kwa kuwa yuko mbele kuliko yule bki wa pili wa mwisho,
(3)Kumwingilia mpinzani kwa kuchepuka kabla ya mpira kupigwa.
Mchezaji huyu atakuwa ameotea.

YAJUE HAYA
Beki wa mwisho katika mpira wa miguu ni golikipa.(Last defender)
Mabadiliko-Substitution
Mchezaji mpya-Substitute
Mchezaji anayetoka-Substituted

Pia tufahamu ya kuwa tunaye mwamuzi au waamuzi wa pembeni,
ambao ni Assistant referees.
Hatuna linesmen siku hizi,kwa kuwa mpira wa miguu unachezwa pia na wanawake.
Hivyo kuweka usawa katika soka,wataalam waliamua kubadili hilo jina la linesman na kuwa ASSISTANT REFEREE.

ENEO ALIPO GOLIKIPA WAKATI WA MCHEZO.
Eneo hili limegawanyika sehemu mbili ambazo ni
1.Eneo la goli.(Goal area)Siyo Kwenye Sita.
2.Eneo la penati(Penalt area)Na siyo kwenye 18

Mchezo wa mpira wa miguu una lugha yake au matamshi yake.
Tuzijue ili tuepuke migogoro isiyo ya lazima katika mchezo huu maarufu duniani.

FAULO NA UTOVU WA NIDHAMU(Fouls and Misconduct)
Mchezaji anayecheza faulo yapaswa aadhibiwe kwa kadi aidha njano au nyekundu
kutegemeana na kosa lenyewe.
Utovu wa nidhamu umegawanyika sehemu nyingi ikiwa ni pamoja na kutumia lugha isiyo ruhusika katika mpira




  •                              ''FOOTBALL IS LIFE'' .

No comments:

Post a Comment