Sunday, August 18, 2013

MPIRA WA MIGUU NI NINI?NA SHERIA ZAKE ZIKOJE?KELELE NA LAWAMA ZISIZO NA MAANA HAZIJENGI SOKA.

Mpira wa miguu pia uitwao soka au kandanda,ni aina ya mchezo ambapo timu mbili za wachezaji kumi na mmoja kila moja hushindana kwa kupigania umiliki wa mpira na kuingiza mpira katika wavu na wapinzani wachezaji hucheza kwa miguu.

Pia wanaruhusiwa kutumia sehemu yoyote ya mwili isipokuwa mikono hairuhusiwi kutumiwa.Mlinda mlango ndiye anayeruhusiwa kutumia mikono.Wachezaji wengine wameruhusiwa kutumia mikono iwapo mpira ni wa kurusha baada ya kutoka nje ya uwanja..

Zifuatazo ndizo sheria zinazotawala mchezo huu
1.Uwanja wa mpira
2.Mpira wa kuchezea
3.Idadi ya wachezaji
4.Vifaa vya wachezaji
5.Mwamuzi
6.Mwamuzi msaidizi
7.Muda utumikao katika mchezo
8.Kuanza na kuanzishwa kwa mchezo
9.Mpira kuwa nje na ndani ya mchetozo
10.Ufungaji
11.Kuotea
12.Faulo na utovu wa nidhamu
13.Pigo la adhabu
14.Pigo la penati
15.Mpira wa kurusha
16.Pigo la kuanzia golini
17.Pigo la kona

Tuelewe kuwa pigo  la adhabu limegawanyika sehemu 2
a.Pigo la moja kwa moja
b.Pigo la kupitia kwa mchezaji mwingine.

Pia tutambue kuwa kelele zisizo na maana hazisaidii kujenga soka.

1 comment: