MSHAMBULIAJI Didier
Drogba ameendelea kuwa mwiba kwa Arsenal akikumbushia enzi zake
alipokuwa na jezi ya Chelsea, baada ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa
miaka 35 leo kufunga mabao mawili na kuiwezesha klabu yake, Galatasaray
kutwaa Kombe la Emirates.
Kweli, ni mashindano ya
kirafiki na hayana maana yoyote katika msimu, lakini lilikuwa kama pigo
lingine kwa kikosi cha Arsene Wenger.
Mfaransa huyo aliwaka
ile mbaya kana kwamba mashindano hayo yana maana yoyote. Alimfokea refa
wa akiba, Andre Marriner baada ya refa Jon Moss kuwazawadia penalti
wapinzani dakika 12 kabla ya filimbi ya mwisho kutokana na Ignasi’s
Miquel kumsukuma mshambuliaji huyo wa Ivory Coast.
Drogba alikwenda mwenyewe kupiga penalti hiyo na kumpeleka upande tofauti kipa Wojciech Szczesny na mpira alipoupiga.
Drogba akafunga tena
zikiwa zimesalia dakika nne, baada ya kupokea pasi ya Wesley Sneijder na
kumuacha Per Mertesacker, kabla ya kumtungua tena Szczesny.
Arsenal ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao katika mchezo huo dakika ya 38, mfungaji Theo Walcott.
Katika mchezo huo,
kikosi cha Arsenal kilikuwa; Szczesny, Jenkinson, Sagna, Mertesacker,
Gibbs/Miquel dk69, Arteta, Ramsey, Oxlade-Chamberlain, Cazorla/Zelalem
dk61, Walcott na Sanogo/Giroud dk61.
Galatasaray Muslera;
Semih, Riera, Chedjou, Eboue, Melo/Sarioglu dk66, Engin Baytar/Gulselam
dk32,Altintop/Colak, dk45, Amrabat, Elmander/Drogba dk45, Umut
Bulut/Sneijder dk45.
Drogba amefunga mabao dakika za lala salama Kombe la Emirates leo
Drogba akimuuza Wojciech Szczesny
Walcott akishuhudia krosi yake ikiipa Arsenal bao la kuongoza
Walcott akishangilia na wachezaji wenzake wa Arsenal
Emamanuel Eboue (kulia) alikuwa Nahodha wa Galatasaray ilipomenyana na timu yake ya zamani leo, Arsenal
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger alivyokuwa baada ya kipigo
No comments:
Post a Comment