Monday, August 5, 2013

KAIZER CHIEFS YAICHAKAZA AZAM FC 3-0

 



KIKOSI KAMILI CHA KAIZER CHIEFS AMBACHO LEO WACHEZAJI WAKE WENGI WALIPUMZISHWA
Azam FC imechapwa mabao 3-0 na wakongwe wa soka la Afrika Kusini, Kaizer Chiefs.

Chiefs maarufu kama Amakosi wameifundisha soka Azam FC katika mechi ya kirafiki iliyochezwa jijini Johannesburg.

Azam ilionyesha soka la ushindani, lakini Amakosi ambao walitumia asilimia kubwa ya wachezaji ambao hukaa benchi walifanikiwa kuibuka na ushindi huo kiulaini.

Mechi inayofuata na Azam FC ni Agosti 7 dhidi ya Mamelodi Sundowns inayonolewa na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Afrika Kusini, Pitso Mosimane.

Baada ya hapo itashuka tena uwanjani kucheza na watukutu wa Afrika Kusini Orlando Pirates siku ya Oktoba 13.

No comments:

Post a Comment