Wednesday, September 25, 2013

JAVIER CLEMENT KUWA KOCHA LIBYA


Libya imeafikiana na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Hispania Javier Clemente kuchukua uongozi wa timu yake ya taifa.
Muhispania huyo aliwasili nchini Libya siku ya Jumaatatu na amekua akijadiliana na shirikisho la kandanda la
Libya.
Rais wa shirikisho hilo Anwar Altashani ameliambia jarida la michezo la Hispania AS kua Clemente ataanza rasmi kazi kama kocha wa timu ya taifa mnamo mwezi wa Octoba.
Clemente mwenye umri wa miaka 63 anachukua nafasi ya Abul Hafidh Erbeesh, aliyejiuzulu mapema mwezi huu.
Kazi yake ya kwanza itakua kujenga hamasa ya timu hiyo baada ya kutolewa katika michuano ya kufuzu fainali za kombe la dunia la mwaka 2014 kwa kuishindwa na Cameroon katika mchuano wa mwisho kuamua timu itakayofuzu.
Clemente aliiongoza timu ya Hispania kati ya mwaka 1992 na 1998, na pia amewahi kua kocha wa Serbia na Cameroon.
Mbali na uzoefu wake kimataifa,Clemente amewahi pia kuongoza vilabu mashuhuri vya Hispania Athletic Bilbao na Atletico Madrid - na mwaka jana alisimamia kwa muda mfupi klabu ya Sporting Gijon .

Libya ni mwenyeji wa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2017.

No comments:

Post a Comment