Mohamed Aboutrika amesaidia Misri kupata ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Guinea katika michuano ya kufuzu kushiriki kombe la dunia kwa timu za Afrika. Hii ni mara ya miamoja kwa Aboutrika kuchezea Misri.
Misri sasa imekuwa timu ambayo haijashindwa katika michuano hii ya kufuzu kwa kombe la dunia litakalochezwa Brazil mwaka ujao.
Tayari Misri ilikuwa imeshinda kundi G na kufika fainali ya michuano ya kufuzu kwenda Brazil.
Lakini Guinea, ambayo ni ya pili kwenye kundi hilo, iliweza kujipatia bao moja ambalo mchezazi wa Misri Adam El-Abd aliingiza kwenye lango lao.
Na ilichukua muda kwa Misri kurejea katika hali ya mchezo mzuri na kisha kuingiza bao lengine mnamo dakika ya 38.
Dakika nyengine nne baada ya kipindi cha mapumziko, mchezaji Kamil Zayatte, aliondoshwa uwanjani na Misri kutumia fursa hiyo huku Aboutrika akiingiza bao lengine ambalo liliiweka Misri mbele
Guinea haikufainikiwa kujikwamua pakubwa baada ya kujiongeza bao lengine moja tu kupitia kwa mchezaji Seydouba Soumah wakiwa wamesalia wachezaji 10 baada ya mwenzao konyeshwa kadi nyekundu
Mohamed Salah aliingza bao la tatu kwa Misri na baadaye mnao dakika ya 83 Guinea mchezaji wa Guinea akapiga shuti kwenye lango lao wenyewe na kuipa Misri ushindi wa mabao manne kwa mawili.
Matokeo hayo yaliipa Misri hadhi ya kuwa timu ya pekee kushinda katika makundi kwa kuwa na pointi 18.
No comments:
Post a Comment